Hii harufu ukeni itakwisha Lini!? 

Kama umekuwa unajiuliza swali hili hii ndio njia pekee na ya haraka itakayokuwezesha kuondoa harufu mbaya  ukeni

Ni kawaida kwa mwanamke kupata harufu ukeni kutokana na hali ya uke kujisafisha kutoa vimelea wabaya. Lakini pale harufu inapokuwa kali sana mfano wa harufu ya shombo ya samaki basi ujue kuna tatizo kubwa. Kutokwa na harufu mbaya ukeni huwa inaambatana na dalili zingine kama kuwasha na kuchomachoma na kutokwa na majimaji au uchafu kama mtindi ukeni.

 Harufu mbaya ukeni kwa kiasi kikubwa husababishwa na bacteria wa vaginosis japo siyo kila mara ndio maana kuna umuhimu wa kutafuta chanzo cha tatizo la kunuka uke. Kama wewe muhanga wa tatizo hili basi tambua kwamba kuna njia za asili unaweza kuzitumia ikiwemo lishe na ukarudi katika hali ya kawaida,kama tatizo litazidi kuendelea basi itatakiwa uende hospitali ili upate uchunguzi. 

Tatizo la kutokwa na harufu mbaya ukeni ni moja ya matatizo yanayowasumbua wanawake wengi nchini na ni tatizo linalokera na gumu kuongeleka kutokana na wanawake wengi kuona aibu na kuhisi ni hali mbaya kwa mtu mwingine kuifahamu.  

Hivi ni Visababishi vya Tatizo la Kuanza kutoka harufu Mbaya Ukeni

.Ukuaji wa bacteria wa vaginosis

Bacteria vaginosis ni chanzo namba moja kinachosababisha uke kutoa harufu mbaya.

Inawezekana ukawa msafi mpaka mwisho lakini ukisumbuliwa na hili tatizo basi lazima uke wako utatoa harufu mbaya.

Kila uke una bacteria ambao wapo naturally kwa ajili ya afya njema ya uke wako,Lakini kama ikitokea hawa Bacteria wakazidi na kuwa wengi kupita kiasi ambacho uke wako unaweza kuhimili ndipo tatizo hili hutokea 

Ukitaka Kujua kuwa unasumbuliwa na bacterial vaginosis utajikuta unapata Dalili zifuatazo  


Ukuaji wa bacteria wa vaginosis ndani ya uke wanaweza kupelekea mimba kutoka, kujifungua kabla ya wakati na kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa mengine ya ngono. dalili mojawapo ya kwamba tayari una maambukizi ya bacteria ni kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu kali mfano wa harufu ya samaki wabichi


           Yeasts Infections

Hili Pia ni Tatizo,lipo kama la Bacterial Vaginosis.tofauti yake ni kuwa kwenye Bacterial Vaginosis waliokuwa wamezidi ni bacteria lakini huku wanaozidi ni fungus candida albicans.

Ni wanawake wachache huwa wanapata Bacterial Vaginosis lakini wanawake wengi lazima wapate Yeast infection japo mara moja katika maisha yao.


Mara nyingi yeasts infection hutokea tu au inaweza kusababishwa na aina ya vyakula au vinywaji unavyokula au kunywa hasa kama vimejaa yeast(vyakula vyote vinavyotengenezwa na hamira,pombe etc) 


Ukitaka kujua kama unasumbuliwa na yeast infection hizi ndizo Dalili zake


Kutozingatia usafi 

Ni wazi kwamba uchafu na kuwepo kwa unyevunyevu sehemu za siri huzalisha harufu mbaya. Kisayansi ni kwamba tezi zilizopo ndani ya mwili (apocrine sweat glands )hutengeneza mafuta kuelekea kwenye maeneo kama kwapa, pua, ndani ya sikio, uke, na kwenye chuchu, bacteria waliopo maeneo hayo huchakata mafuta haya na hivo kuzalisha harufu kali. Uvaaji wa nguo zilizobana na uzito kupita kiasi huchangia kuhifadhiwa kwa jasho kwenye mikunjo ya ngozi na hivo kuleta harufu.

Mabadiliko ya Homoni 

Mabadiliko ya homoni kutokana na mzunguko wa hedhi huweza kuchangia harufu mbaya ukeni,wanawake wanaokaribia kukoma hedhi wako kwenye hatari zaidi kwani homoni ya estrogen hupungua sana hivyo kusababisha tishu kuwa na tindikali kidogo 

Ugonjwa wa Trichomoniasis 

Trichomoniasis ni moja ya ugonjwa wa ngono unaosababisha harufu kali ukeni. Ugonjwa huu husababishwa vimelea na huambatana na kutokwa na uchafu ukeni,kuwasha, na maumivu makali wakati wa kukojoa. trichomoniasis inaweza kuwaathiri wajawazito na kuleta hatari ya mimba kutoka. Kama utagundua una Trichomoniasisi basi wewe na mwenza wako mnatakiwa kutibiwa. Hakikisha pia unatumia condom vizuri kila unapofanya ngono kama kinga dhidi ya magonjwa


Vaginal cervical cancer Cancer { Kansa ya  Uke / Kansa ya Mlango  wa Kizazi }

Unapokuwa una kansa ya uke au kansa ya mlango wa kizazi ni kawaida kutokwa na maji maji yenye harufu mbaya ambayo ni sehemu ya dalili za kansa ya uke,.Unapojiona kuwa una tatizo la uke kutoa harufu mbaya,ni heri na itakuwa busara ukienda hospitali,kupima na kama ni kansa ya mlango wa kizazi itakuwa sio ngumu kuitibu kama ukiwahi mapema kuanza matibabu 

Zipo sababu nyingi tu zinazosababisha kutokwa na harufu ukeni. kwa kuzifahamu zaidi namna unavyoweza kuondoa haraka harufu ukeni wasiliana na wataalamu kwa ushauri na tiba