Ngarisha Ngozi yako kwa Nguvu ya Asili na Kuifanya iwe Laini na Ng'avu Boresha afya  ya Ngozi kwa Tiba isiyo na Mazara






Wekeza katika ngozi yako kwa kuwa itakuwa ikikuwakirisha mbele za watu kwa muda mrefu

Program Hii itaondoa Mikunjo na Kukuweka Mrembo siku Zote

Tunaboreshaje Afya ya ngozi yako 

Vitu vingi tunavyoviona juu ya ngozi zetu ni matokeo ya vile vinavyoendelea ndani uzuri wa ngozi yako na ubora wake vinahusiana sana na afya ya mwili wako kwa ujumla 

---------------------------------------------

Jinsi ambavyo chunusi Utokea 


Chunusi ni katika matatizo ya ngozi ambayo huathiri watu wengi wakati fulani. Husababisha madoa, ngozi ya mafuta na wakati mwingine ngozi ambayo ukiigusa unahisi hisia za moto au uchungu. Chunusi (kwa Kiingereza: acne vulgaris) ni hali ya muda mrefu ya ngozi inayodhihirika kwa madoa meusi, madoa meupe, ngozi yenye mafuta na wakati mwingine kovu.


Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso, kifuani na hata mgongoni. Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani bacteria. 

Maambukizi zaidi ya chunusi hutokea pale ambapo vijidudu yaani bakteria vinaposhambulia vishimo vilivyoziba; hapo kivimbe ambacho watu wengine huita upele hujitokeza pale ambapo Sebum, bacteria, seli za ngozi na seli nyeupe za damu zinapochanganyika na kujikusanya katika vishimo vya jasho vilivyoziba na eneo husika hupata vivimbe au vipele ambavyo tunaviita chunusi. 


Magonjwa

Kuna wakati watu wanapata chunusi kwa sababu ya matatizo yanayohusiana na afya zao, unaweza kumkuta mtu ana upungufu wa baadhi ya vitamini au ana tatizo la kiafya linalopelekea apate matatizo kwenye ngozi mfano ukiwa na kisukari ni rahisi kupata chunusi. Ngozi yako ni kioo kinachoonesha mambo yanayoendelea ndani hauwezi ukawa na afya iliyokua dhaifu halafu utegemee ngozi iwe nzuri. Magonjwa yatokanayo na matatizo katika homoni (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana.

Madhara ya tokanayo na chunusi 

Aina za madoa ya chunusi 

Kuna aina 6 kuu za madoa zinazosababishwa na chunusi 

Kama upo tayari kupokea ushauri ni kwa jinsi gani utaweza ufanya ili kuweka ngozi yako. katika muonekano nadhifu  na wakupendeza na pia kama una chunusi utaweza kuziondoa kabisa. ni vyema ukatutafuta ili uweze kupata msaada kutoka kwetu. karibu kwa msaada