Tiba ya kutokupata hedhi
Hedhi ni matokeo ya kubomoka kwa ukuta wa kizazi ulioandaliwa kushikilia mimba lakini kwa vile mimba haijashika ukuta huu humeguka na kutolewa nje kama damu ya hedhi.
Wanawake huanza hedhi katika kipindi cha kubalehe kuanza miaka 10 mpaka 16 na hedhi huendelea mpaka pale wakifikia menopause(kukoma hedhi) miaka 45 mpaka 55.
Hedhi inapoanza kutoka kwenye balehe inaweza kuchukua mpaka miaka miwili ili mzunguko kukaa sawa. Baada ya balehe hedhi hutengemaa na siku za mzunguko huanza kufanana.
Japo kwa baadhi ya wanawake hata baada ya balehe kupita hedhi haikai sawa na kiwango cha damu inayotoka kinakuwa kidogo ama kingi kupita kiasi hii ndio hupelekea mvurugiko wa hedhi.
Nini kinasababisha Hedhi Kuvurugika?
Mchango wa homoni kuvurugika: Homoni au vichocheo vikuu zinazoratibu mpangilio wa hedhi yako ni estrogen na progesterone, inaweza kuchukua miaka mingi kwa homoni hizi kuwa na uwiano sahihi. Vihatarishi amavyo vinapelekea kuvurugika kwa homoni na hatimaye hedhi kuvurugika ni pamoja na
Matumizi ya uzazi wa mpango wa kisasa kama sindano, vidonge na vijiti
Uzito mkubwa kupita kiasi na kitambi
Kupungua uzito kupita kiasi
Msongo wa mawazo
Changamoto za kushindwa kula vizuri na hivo kukosa virutibishi muhimu
Mazoezi makali mfano riadha
Kuugua maambukizi kwenye kizazi(PID) kwa muda mrefu: endapo maambukizi haya yasipotibiwa mapema yanaweza kuathiri mirija ya uzazi pamoja na kizazi kwa ujumla na hivo kuvuruga mpangilio wa hedhi,
Vimbe kwenye mayai(polycstic ovarian syndrome);mfuko wa mayai kwa mwanamake huitwa ovary na mifuko hii huwa miwili kushoto na kulia. Kila mwezi mwanamke hutoa yai moja kwenye kikonyo chake katika upande mmoja ili liweze kurutubishwa, inapotokea mayai kugoma kutoka kwenye mfuko ndipo uanageuka kuwa vimbe zenye maji (cyst) zikiwa nyingi huitwa polycyst. Changmoto hii ndio chanzo kikuu cha mwanamke kuvurugikiwa hedhi.
Saratani kwenye kizazi inaweza kusababisha mwanamke kupata hedhi nzito sana ama hedhi katikati ya mzunguko wake
Matatizo ya tezi ya shingoni (thyroid gland), tezi hii ndio inayoratibu utolewaji wa homoni za estrogen na progesterone, tezi ikipata hitilafu inapelekea kuvurugika kwa homoni na hivo hedhi pia kuvurugika.
Kuvimba kwa kiazi(endometriosis): hali hii hutokea pale seli za ndani ya ya mfuko wa mimba zinapota na kutoka nje ya mfuko wa mimba, hali hii hisababisha maumivu makali wakati wa hedhi lakini pia yaweza kusababisha mabaki ya hedhi kwenye kizazi.
Baada ya kutumia tiba yetu tegemea kupata matokeo haya
Homoni kubalansi
Mzunguko wa hedhi kurekebika na kuanza kupata kila mwezi
Hedhi yako kuwa nyepesi ya kawaida
Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi kuisha kabisa na
Kizazi kuimarika sana hata kuongeza chansi ya kushika mimba kama wewe ni muhanga wa kukosa mimba kwa muda mrefu